म्सादा तुतानी वाजमेनी

Hii ni mimi mwenyewe imenitokea jamani si kama mtu mwingine yeyote hapana nilipeleka barua ya uchumba kwa msichana mmoja hivi kwa kuwa tayari tulishakubaliana kwamba nipeleke tu barua,Mimi nikatuma mshenga kama ilivyoada ya waislamu wote umuonapo mchumba na mkikubaliana unapeleka barua basi nikafanya hivyo bila kujua kwamba mshichana alikuwa anakubali tu ili anilidhishe na moyo wangu ulidhike,kumbe msichana alikuwa na byfrend kitu ambacho mimi nilkuwa sijui ikafika siku ya kusomwa ile barua bila wao wenyewe kujua chochote kwambqa kwenye kile kikao kuna mama yangu mdogo,yule msichana akakataa katukatu kwamba awezi kukubali barua yangu kwa kuwa yupo aliyempenda zaidi kuliko ya mimi kumba masikini ya mungu bila wao kujua chochote kile kwamba kuna mtu anawafanyia ushushushu basii kwa kuwa mimi nilipeleka barua siku ya jumatano na yeye mwenzangu aliahidi atapeleka jumapili basi ile ya kwangu ikawekwa pending kwa kusubiri iyo nyingine wakapanga cha kujibu masikini ya mungu mshenga wangu akaambiwa kwa kuwa msichana amelipiwa ada na kaka ake mkubwa hawataweza kukubali barua yangu kwasababu wakikubali mdogo wao atashindwa kusoma,kabla mshenga ajarudi mama yangu mdogo akaniletea salamu za kule mimi na mama yangu mdogo tukamtuma mshenga akienda asisikilize la mtu yeyote yule arudi tu na barua ndio cha msingi.
basi nikarudishiwa barua yangu basi kuanzia hapo nikawa pombe mtu masikin mtoto wa mosi mlaponi na hiyo ambayo nilikuwa natumia kunywa ni hapo karibu na huyo msichana
siku moja nimkaa sina hili wala lile nikaletewa kimasage kutoka kwa binti ambaye mimi mwenyewe sikumfahamu imeandikwa hivi :abdallah naomba samahani yule ni shetani tuu basi mimi nikamfuata yule msichana tukaanza uusiano kati ya mimi na yey lakini sas yule msichana mwenzenu ananiendesha sana kila nikisimama tu na msichana kesi sasa nashindwa kuelewa mbona mwanzo alinikataa na saa hizi ananisumbua?
na huyu msichana niliamua bora nimuache mama yake kanijia juu na hapohapo tayari ni9meshapata mcumba mwingine na mama yake kama hivyo ameanza kunisumbua kwamba nisimuache mwanaye sasa mimi nifanyeje na mbona mama yake ajamkalia kohoni yule jamaa wa mwanzo kabisaa au kwasababu mimi ananijuwa?

msaada kwenu wadau wangu.

JAMANI MEDY

KWA TAARIFA NILIZOZIPATA KUWA ALIYEKUWA MUME WA MBUNGE WA VITI MAALUMU KUPITIA TIKETI YA CCM AMINA CHIFUPA AMBAYE NAYE ATUPO NAYE TENA MOHAMED MPAKANJIA ALMAARUFU MEDY AMEFARIKI DUNIA JANA MAJIRA YA SAA TISA ALASIRI KWA UGONJWA WA ENIMONIA TAARIFA ZILIZOFIKA ZINASEMA KWAMBA ALIKUWA AKISUMBULIWA NA MARADHI HAYO SASA KAMA SIKU TATU AMBAPO JANA NDO ILIKUWA TAMATI.
MUNGU AMETWAA NA MUNGU AMETO.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMEEN.

MSAADA TUTANI

Hii ni mimi mwenyewe imenitokea jamani si kama mtu mwingine yeyote hapana nilipeleka barua ya uchumba kwa msichana mmoja hivi kwa kuwa tayari tulishakubaliana kwamba nipeleke tu barua,Mimi nikatuma mshenga kama ilivyoada ya waislamu wote umuonapo mchumba na mkikubaliana unapeleka barua basi nikafanya hivyo bila kujua kwamba mshichana alikuwa anakubali tu ili anilidhishe na moyo wangu ulidhike,kumbe msichana alikuwa na byfrend kitu ambacho mimi nilkuwa sijui ikafika siku ya kusomwa ile barua bila wao wenyewe kujua chochote kwambqa kwenye kile kikao kuna mama yangu mdogo,yule msichana akakataa katukatu kwamba awezi kukubali barua yangu kwa kuwa yupo aliyempenda zaidi kuliko ya mimi kumba masikini ya mungu bila wao kujua chochote kile kwamba kuna mtu anawafanyia ushushushu basii kwa kuwa mimi nilipeleka barua siku ya jumatano na yeye mwenzangu aliahidi atapeleka jumapili basi ile ya kwangu ikawekwa pending kwa kusubiri iyo nyingine wakapanga cha kujibu masikini ya mungu mshenga wangu akaambiwa kwa kuwa msichana amelipiwa ada na kaka ake mkubwa hawataweza kukubali barua yangu kwasababu wakikubali mdogo wao atashindwa kusoma,kabla mshenga ajarudi mama yangu mdogo akaniletea salamu za kule mimi na mama yangu mdogo tukamtuma mshenga akienda asisikilize la mtu yeyote yule arudi tu na barua ndio cha msingi.
basi nikarudishiwa barua yangu basi kuanzia hapo nikawa pombe mtu masikin mtoto wa mosi mlaponi na hiyo ambayo nilikuwa natumia kunywa ni hapo karibu na huyo msichana
siku moja nimkaa sina hili wala lile nikaletewa kimasage kutoka kwa binti ambaye mimi mwenyewe sikumfahamu imeandikwa hivi :abdallah naomba samahani yule ni shetani tuu basi mimi nikamfuata yule msichana tukaanza uusiano kati ya mimi na yey lakini sas yule msichana mwenzenu ananiendesha sana kila nikisimama tu na msichana kesi sasa nashindwa kuelewa mbona mwanzo alinikataa na saa hizi ananisumbua?
na huyu msichana niliamua bora nimuache mama yake kanijia juu na hapohapo tayari ni9meshapata mcumba mwingine na mama yake kama hivyo ameanza kunisumbua kwamba nisimuache mwanaye sasa mimi nifanyeje na mbona mama yake ajamkalia kohoni yule jamaa wa mwanzo kabisaa au kwasababu mimi ananijuwa?

msaada kwenu wadau wangu.

MIMI NA BOSI TUKIWA KAZINI


JAMANI WADAU WANGU HAPA NI OFISINI KWANGU NA HUYO MNAYEMUONA NI BOSI WANGU HAPA TUKICHAPA MZIGO.LAKINI LEO BINAFSI NIMECHUKIZWA SANA NA MWADADA MMOJA HAPA OFISINI SIWEZI KUMTAJA JINA LAKINI MAMBOYOTE NAMUACHIA MUNGU ABDALLAH PICHA NA HISANI YA SAIDI HADJI.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO BWANA JAKAYA MRISHO KIKWETE


RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AMELIHUTUBIA TAIFA JANA NA MENGI SANA KAYAZUNGUMZIA LAKINI NAFIKIRI LILE LA MUHESHIMIWA ZOMBE KALIZUMZIA VIZURI SANA KIASI KWAMBA LIMEKUWA NI KIVUTIO NANUKUU ALICHOSEMA" NILIKUWA NIMESAFIRI SIKU NILIYORUDI KWASABAU TIBAIGANA ALIKUWA YUPO LIKIZO KWA HIYO ZOMBE ALIKUWA AKIKAIMU NAFASI YA TIBAIGANA NIKAMUULIZA KUHUSU SWALA LA UJAMBAZI AKANAMBIA SWALA UJAMBAZI LINAENDA VIZURI HATA JANA TUMEUWA MAJAMBAZI LAKINI BAADA YA MUDA SI MUREFU NIKASIKIA SIO.MZEE JAKAYA FANYA KAZI BWANA KWA KWELI HATA MIMI ABDALLAH NGATUNGA INANIUMA SANA SWALA LA ZOMBE HAYA KAZI KWENU.

RAISI JAKAYA KIKWETE ATALIHUTUBIA TAIFA LEO.


HABARI ZA KUAMINIKA KUTOKA KWENYE OFISI ZA IKULU LEO HII MAJIRA YA SAA MBILI NA NUSU USIKU RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ATALIHUTUBIA TAIFA MENGI YALIYOMO MAPYA NI KWAMBA RAAISI LE HII PIA ATAJIBU MASWALI YOTE UTAYOYAULIZA KUPITIA SIMU LIVE HII NI MPANGO MPYA AMBAO HAKUNA RAISI WOWOTE WA AFRICA KAFANYA KITU KAMA HICHO
MPO TAYARI KUULIZA MASWALI YENYE KLUJENGA, USHAURI NA MASWALA UNAYOYAONA MUHIMU YEYE KAMA RAISI KUJIBU MUULIZE THEN KAMA UNATAKA KUULIZA KUPITIA MAIL ANDIKA UJUMBE WAKO KISHA TUMA KWENDA pb@cloudsfm.co.tz.

DIAMOND MOTORS LTD AU MITSUBISHI MOTORS


JAMANI HIYO NI NEMBO YA MITSUBISHI MOTORS PALE AMBAPO MIMI NAFANYA KAZI KARIBUNI SANA.
TUNAUZA MAGARI YA MITSUBISHI,TUNAUZA SPARES ZA MAGARI YA MITSUBISHI TUNAFANYA SERVICE YA MAGARI YA MITSUBISHI NA MENGINEYO MENGI KWA MAULIZOZAIDI UNAWEZA KUTUMA EMAIL YAKO KUPITIA diamond@rajani-group.com UTAJIBIWA MUDA WOWOTE ULE MASAGE YAKO ITAPOINGIA KWA TAARIFA NI KWAMBA TUMELETA GARI MPYA MITSUBISHI PAJERO NA MITSUBISHI PICKUP SPOTERO.

SIKU YA HARUSI YA DADA ANGU PALE KANISANI ST ALBANI POSTA MPYA



href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHE3hjihIM0RkM9rBsvsR1f16X3B58fnvbeDr8Uc5FsQsxUBD8UL_LPGFaPLGT-IYkA-xh9m3XwW_qo9HbImrHaEfDqziKsx8bg5oOJMwocy4qctPPJku8KsEOkOltltj7DBm5mblM2Kw/s1600-h/UKUMBI.jpg">


href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgQkimVkUSSXunIit_jrDIgn2BjS_JjRzdrVfQkQcM2vaRuHdnkLZU2cncum-cqtBNi_JA7i9ABoYaoUj6lepzczpWMZC4kagF40QOPA3UNlxUtkB7sDz_xK9BG3PN0-GiDKPvE_e0hnzs/s1600-h/MEZA+KUU.jpg">


href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOxTL67I8FaF-o5bV2OQSsxPtLSfNrELLOrxWtGERncKvfKp-5ZvHptet7ta4BDeQBLb85vptDhMIlaapmuxtD_0W2Z5bTrCHnoDgl4aXkub3jj18aKTjczvLSnQw-ZVNRJSHXEn01MVw/s1600-h/MR+MOSES+AND.jpg">


href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9yEkwoiN59qWixfMPh4dq9zW2MUdT8J5knEGS8u55k8gSLZkR_Zq_eF91TL3VJnee1-ltC7kA3-EmAThDWSSdeKhmWdVDK6bsfNY8T16byaR1vredexZxxV5AVG8XWZYPZFZzxa69wCU/s1600-h/KULA.jpg">


href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRub6VVG_DVlpwsZaStZ3L4Ccm-sGd3s85MCI_7jFTr22Tv-MRx7KmbCNPPxIjfMIjt7IUiBFLte_0WeU6y49iqwH3vtHVA_h-sjygxZwXk4mcbYRQzAhxqNpyvZVwOBVoLLzPTpOEHmc/s1600-h/KEKI.jpg">


href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjff-gKkaCPsS-HzsBFQZU8tdYkEsgLcIu5kPkGc5bvdGM7DUqeOXlISDw5MqOBOBof9t6t_CxhoiTxcjBlMVXJ3hzDt5RRbBTj7BnCgp0QGCrl79fcuNGui_qBYZ6fE8ZzKYF75D6iyVQ/s1600-h/KANISANI.jpg">


href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgowEdw7tC8CXtVgIkWF1qUlFS8WQRze1uj1QFYgsbDLeamHlN_pqpYEcrPg8p5QdR5EAG2qApkcFa_9wPnWxe0wg4LJpboS297UFEzwxuLUZ5QhkOOzdiL0Otam6nNx5AmGBN4XaL6rg0/s1600-h/KAKA+TUMAI.jpg">


href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj8wxI4VUyi0T5MaxtUpIFYf0L1HlJ3GR4IePKpS4mWWY6rchOkNzarY6lkcJDkSpmam8T6iXTrqO7wNbPhSoNLQnzDdGh8xo4MAtTCgvu5EudVDmZ2v3Fij9-FiFpYMWcNLxYL3c6DLnM/s1600-h/CASSA.jpg">


href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0_IwIcwLNBwhmQnZe67qRX4HJXusxEuLcb3PpIGGhN8cPN4JIzQYhNtpicP_IkI4-4h5P6U-05sY5_lqTQcTzXs39iuQ_-U_nb-PAQ4JGp6nsUlvFYN4cqznK8Z0W-b3TnpEpoOWulVM/s1600-h/ASKOFU.jpg">


HAPA DADA AKIWA ANAHAPA KWAMBA HATAMUACHA MSHIKAJI ATA AKICHOKA

NAWEWESEKA SANA JAMANI MWENZENU

NIPO KATIKA WAKATI MGUMU SANA HASA KUHUSIANA NA SWALA LA MAPENZI,MWENZENU BADO PIGO LANGU HALIJAFUTIKA TANGU PALE MWAKA 2007 NILIPOONDOKEWA DUNIANI NA KIPENZI CHANGU CHA ROHO ARAFA RASHID TANGU HAPO MWENZENU NAKUWA NIPO KWENYE WAKATI MGUMU SANA SIJUI HATA NIFANYEJA,KWASABABU KILA MSICHANA NINAYE KUWA NAYE HAFAFNANI NA MPENZI WANGU AMBAYE KANITOKA SIJUI NIFANYEJE MWENZENU,KUNA KIPINDI NAHISI HATA MWENYEZI MUNGU KANIONEA HAKUNA MSICHANA NILIYEKUWA NAMPENDA KAMAA YEYE SASA JAMANI NAJARIBU KUTAFUTA NAMBA YA SIMU YA MZEE WA PILOTOP AMANI MISANA MWENZENU ANAWEZA AKANIADVICE CHOCHOTE MWENYE NAMBA YA HUYU JAMAA NAOMBA ANISAIDIE.

WAKATI NAELEKEA VEKESHENI MOROGORO NILIKUTANA NA HII

MUME NA MKE WALIKUWA WAMEKAA SITI MOJA SASA INAVYOONEKA WALIKUWA NA KAUGOMVI TANGU NYUMBANI WAKATI TUPO MBUGA ZA WANYAMA PALE MIKUMI HALI ILIKUWA HIVI MUME ALIWAONA NYATI KWA SAUTI KUBWA ALISIKIKA AKISEMA AKIMWAMBIA MKEWE MUME" UMEWAONA NDUGU ZAKO AKIMAANISHA WALE NYATI BILA KUSITA MKE NAYE AKAJIBU NDIO WALE SI WAKWE ZANGU BASI ZIMA HOI.

WAPI NNCHI INAELEKEA SASA


HIVI NDIVYO ILIVYO SASA BAADA YA JUMUIYA YA KANISA KATOLIKI KUTOA WARAKA WAO SASA NI DHAMU SURA IMAMU KWA UPANDE WA WAISLAMU SASA SWALI NAULIZA TUNAELEKEA WAPI? KAMA TUMESHAANZA KUJIBAGUA HIVI TUTAFIKA? NAKUMBUKA MANENO YA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIZUNGUMZA KWENYE MKUTANO WAKE MMOJA KUHUSIANA NA SWALA LA KUBAGUANA JE YEYE MWALIMU LEO ANGEKUWEPO INGEKUWAJE?

HAPA NIKIWA OFISI


HAPA MZEE ALINISHITUKIZA TU TOA MAONI YAKO NIPO KWENYE POZI GANI?

MAN U FC VS ARSENAL

MANCHESTER UNITED VS ARSENAL ZINAKUTANA TENA LEO KWENYE LIGI KUU YA UINGEREZA.MECHI HIYO ITAKUWA YA KUKATA NA SHOKA PALE ITAPOWAKUTANI WABABE HAO.MANCHESTER UNITED IKIWA NA RECOD YA KUWAFUNGA ARSENAL GOLI NNE KWA MOJA WASHIKA BUNDUKI HAO WA LONDON WANAINGIA UWANJANI LEO WAKIWA NA MATUMAINI YA KUWAFUNGA MAN U FC,MATUMAINI HAYO YANATOKANA NA KUUZWA KWA WAHEZAJI MAHIRI WA MAN U FC CRISTIANO RONALDO PAMOJA NA CARLOS TEVEZ AMBAPO MECHI ILIYOPITA WABABE HAO WAWILI NDIO WALIYOIBEBA MAN U FC.

LEAGE YA ENGLAND INAENDELEA TENA LEO MAJIRA YA JIONI SAA MOJA ZA KITANZANIA


HILI NDIO DIMBA AMBALO LEO TUTASHUUDIA WABABE WAWILI WA LEAGE YA ENGLAND WAKITOANA JASHO AMBAPO LEAGE IKIONGOZWA NA WABABE KUTOKA KWENYE JIJI LA TOTENHAM AMBAO WANA POINTS 9 WAKIWA NA MICHEZO MITATU IKIFUATIWA NA WABABE KUTOKA CHELSEA AMBAO NAO WANA POINTS 9 YA TATU NI ARSENAL AMBAYO NAYA INA POINTS SITA IKIWA SAWA NA MAN U FC.

MAN U FC VS ARSENAL


KWA WAPENZI WA ARSENAL JUMAMOSI ANDAENI MACHOZI KABISAAAAAAA MAANA AKE SI MMEMUONA GALASA KASHAANZA SHUGHULI YAKE.

LIGI KUU YA ENGLAND ILIANZA RASMI NAYO






HAPA NI SIKU AMBAYO MAN U EC TULIPOWANYUKA GOLI TANO WIGAN.

LIGI KUU BARA IMEANZA HUKU YANGA IKIBANWA NA AFRICAN LYON



HAPA JERISON TEGETE WA YANGA AKIJARIBU KUMTOKA BEKI WA TIMU YA AFRICAN LYON.

KITIMTIM CHA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA IMEANZA JANA HUKU TUKISHUUDIA VIWANJA KADHAA VIKITIMKA VUMBI NINA MATOKEA YA MCHEZO KATI YA YANGA KUTOKA WILAYA YA ILALA IKIKUTANA NA AFRICAN LYON KUTOKA TEMEKE KWENYE DIMBA LA UHURU AMBAPO MECHI HIYO ILIENA SARE YA MOJAMOJA. KATIKA DIMBA LINGINE LA SONGEA IKIWAKUTANISHA WAKONGWE WAWILI WA LIGI HIYO MAJAMAJI KUTOKA SONGEA NA SIMBA SPORS CLUB KUTOKA WILAYA YA ILALA DAR S SALAAM AMBAPO NGOMA ILIENDA VIZURI KWA WEKUNDU HAO WA MSIMBAZI AMBAO WALITOKA KIFUA MBELE BAADA YA KUSHINDA GOLI MBILI BILA.KWA MECHI KAMILI FUATILIA BAADA YA MUDA KIDOGO NTAWALETEA HABARI KAMILI.

MSICHANA AJIFUNGUA BILA MTU YEYOTE KUFAHAMU

MSICHANA MMOJA ANAYEKADIRIWA KUWA NA MIAKA KATI YA 24 MPAKA 28 AMEJIFUNGUA SALAMA HAPO NYUMBANI KWAO TANDIKA MTAA WA MUWALE NYUMBA NO 44 TUKIO HILO LILITOKEA MAJIRA YA SAA TATU USIKU TAREHE 22/07/2009 BAADA YA MSICHANA HUYO KUJIFUNGIA NDANI BILA MTU YEYOTE YULE KUJUA CHOCHOTE KILE NA KUJIFUNGUA MSICHANA HUYO INASEMEKANA KUWA ALIKUWA AKIFANYA KAZI KWA MAMA MMOJA AITWAYE MAMA KURWA NA MASHUUDA WA TUKIO HILI WANASEMA HAKUNA HATA MTU MMOJA ALIYEKUWA AKIFAHAMUM KWAMBA HUYU MSICHANA ANGEKUWA NA MIMBA.

DAH HUYU DADA ETU NAYE KAZIDI KHA! SASA HII STYLE GANI?

OMSyvpD7AFs/Sl7w-VK7vQI/AAAAAAAAACg/R_MnCEi_-Bo/s1600-h/untitled.bmp">alt=""id="BLOGGER_PHOTO_ID_5358985560243027202" />

DAH HII NI NOMA.

MANCHESTER UNITED



kwa asiyejuwa jamani ni mpenzi wa MAN U FC mpaka naudhi yani dah!

TUNDA MAN SPACK WAJIUNGA TMK WANAUME FAMILY


JUU PICHA NI TUNDA MAN NA SPACK

KWA HABARI NILIZOZIPATA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KUWA WASANII HAO WALIOANZIA LAFAMILIA MPAKA KUJA TIPTOP CONECTION AMBAO SASA KIUJUMLA WOTE WAMEAMUA KUUNGANISHA JESHI LA TMK.WASANII WENGINE WALIOUNGA MKONO MUUNGANYIKO HUO NI CHEGE,STICKO,MADEE,NA WENGINEO WENGI.

JAMANI MAFUA YA KITI MOTO YAPO BONGO





Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, leo imetoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa hatari wa mafua makali ya nguruwe (Swine Influenza/ FLU) hapa nchini.
Wizara hiyo pia imewataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa juu ya maambukizi ya ugonjwa huo.
Tamko hilo limekuja kufuatia kubainika kuwepo kwa mgonjwa mmoja ambaye amelazwa katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili akiugua ugonjwa huo.
Akitoa tamko hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika wizarani hapo leo , Naibu Waziri katika wizara hiyo Aisha Kigoda, alisema kuwa mgonjwa aliyelazwa Muhimbili ni mwanafunzi , raia wa Uingereza aliyewasili hapa nchini kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK.Nyerere Dar es Salaam, Julai 4, mwaka huu, akitokea London, Uingereza, na ndege ya shirika la Kenya Airways, ambayo ilipitia Nairobi kabla ya kutua Tanzania.
Waziri Kigoda alisema kuwa, mgonjwa huyo ni pamoja na kundi la kwanza la wanafunzi wenzake 15 na walimu wanne. Jumla ya wanafunzi wanaotarajiwa kuja nchini ni 350, kwa ajili ya safari yao ya mafunzo na kupanda mlima Kilimanjaro wakati wa kipindi cha majira ya joto.
Alisema, mgonjwa huyo aligundulika mara moja alipowasili uwanja wa ndege Dar, na kujaza fomu zinazomtambulisha abiria yoyote mwenye dalili za ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa mgonjwa huyo baada ya kutua Dar alionekana kuwa na dalili za homa kali, mafua, kuumwa koo, kupiga chafya pamoja na mwili kuwa dhaifu.
Alisema wataalamu wa afya wa uwanja wa ndege, wakishirikiana na wataalamu wa wizara yake makao makuu, walimchukua mgonjwa huyo na kumweka katika chumba maalum na kuchukua sampuli ambazo zilipelekwa maabara iliyopo kwenye Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa na Binadamu (NIMR) ambapo vipimo vilionesha dhahiri kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na vimelea vya mafua makali ya nguruwe.
Waziri Kigoda alisema sampuli zingine zilipelekwa katika maabara inayotambuliwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) iliyopo Nairobi, Kenya, ambapo pia ilithibitika kuwa mwanafunzi huyo ana virusi vya ugonjwa huo.
Alisema mgonjwa huyo alipatiwa matibabu mara moja na kwa sasa amelazwa katika wodi maalum ya magonjwa ya kuambukiza , Muhimbili, ingawa alisema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri.
Waziri huyo alidai kuwa uchunguzi pia ulifanywa kwa wanafunzi wenzake na walimu wao na hakuna aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Taarifa za kupiga hodi kwa ugonjwa huo hapa nchini zimeonekana kuwatia hofu wananchi wengi, baada ya vyombo vya habari kuripoti juu ya kuwepo kwa mgonjwa mmoja anayeugua ugonjwa huo.

JAMANI TUJIHADHARI NA HIZI

NIMEKUTANA NA HII KWENYE MAIL YANGU JAMANI JIHADHARINI KWA WALE WENYE MAIL MSITOE AKAUNTI NAMBA ZENU KWA WATU KAMA HAWA WASANII TU HAWA WA MJINI.


VERY URGENT
FROM MR. HASSAN BILLY,
GREETINGS.

PLEASE, I WILL LIKE YOU TO CONTACT ME THROUGH MY PRIVATE EMAIL ADDRESS: (mr_hbillya2@voila.fr )

Complement of the day to you and your beloved FAmily, I apologize for this intrusion, I decided to contact you through email due to the urgency involved in this matter. Do not be astonished for receiving this mail. Please, I seek your permission and would want to get myself introduce to you. I am Mr.Hassan Billy. I work with BANK INTERNATIONAL OF BURKINA (BIB).

I need your co-operation in receiving USD9.5M that has been in a dormant account with my bank for over 6years which belongs to one of our foreign customer who died along with his entire family in a plane crash that happened in Kenya, East Africa. I will provide you with detailed informations on the modalities of this operation once I have your interest but I must say that trust flourishes business. Therefore let your conscience towards this proposal be nurtured with sincerity and I will not fail to bring to your notice that, this transaction is hitch-free risk and you should keep this transaction (TOP SECRET).

I agree that 35% of this money will be for you as a foreign partner, in respect to the provision of a foreign account, and 65% would be for me, thereafter I will visit your country for disbursement according to the percentage indicated. Remember, you must apply first to the bank as relation or next of kin of the deceased, indicating your 1) Bank name, 2) Your bank account number, 3) Your private telephone and fax number for easy and effective communication and my career as a banker, I will bring you up to date with all the informations as soon as I hear from you but If I don 't hear from you within a certain period, I will assume you are not interested.

Please, I want you to visit the website below for more informations about the plane crash and the Deceased DR.GEORGE BRUMLEY AND HIS FAMILY.

www.cnn.com/2003/WORLD/africa/07/20/kenya.crash/index.html
www.news24.com/News24/Africa/News/0,,2-11-1447_1390626,00.html

Meanwhile, If you are willing, capable and honest for this transaction, Kindly indicate your interest by sending a response to my e-mail address at: (mr_hbillya2@voila.fr )

Yours Truely,
Mr. Hassan Billy

kisa cha kweli kabisa

Nimehadithiwa kisa kimoja cha kweli na cha kustaajabisha ambacho kimeniacha na maswali mengi na mwisho nikamuuliza aliyenihadithia; “huyo jamaa hakuwa jini kweli? kisa chenyewe nimehadithiwa na dada mmoja aged between 35 – 40 ambaye hapendi nimtaje jina. Alinihadithia kama ifuatavyo:

Mambo? (naishi nae jirani), nina stori nataka nikupe, maana mimi mwenyewe nimeshangaa na mpaka sasa hivi siamini kilichotokea. Wiki iliyopita nilikwenda Morogoro, wakati naondoka hapa nyumbani (anakaa Ilala) kwenda Ubungo nilichukua teksi. Wakati naondoka nilikuwa na jumla ya shilingi 280,0000.

Nilichukua shilingi 30,000 nikaweka kwenye pochi ndogo kisha nikaweka kwenye sidiria, iliyobaki 250,000 nikaweka kwenye bahasha halafu nikaiweka kwenye mkoba wangu ambao nilipokuwa kwenye teksi, niliuweka kwenye kiti cha abiria cha nyuma.

Huyo dereva huwa namuona tu, kwani gari lake huwa analaza jirani yetu, lakini simjui vizuri. Tukiwa tunaelekea ubungo stendi, nilikumbuka simu yangu, nilipojisachi nikaona sina, lakini nilikuwa na uhakika nilipanda nayo, nikamuomba dereva aipige simu yangu ili kama imeangukia ndani ya gari niione.

Nikampa namba yangu akaipiga, kweli ikaita kutoka chini ya kiti nilichokuwa nimekaa. Nikaiokota kisha nikaiweka vizuri tukaendelea na safari yetu hadi Ubungo, tulipofika nikamlipa dereva nauli yake tukaagana. Mimi moja kwa moja kwenye basi hadi Morogoro.

Nilipofika nyumbani Morogoro, nikafungua mkoba wangu ili nitoe ile bahasha yenye 250,000, lakini sikuiona, nikajaribu kupekua vizuri kila mahali lakini wapi, moja kwa moja nikajua ile bahasha yenye pesa nimeibiwa.

Lakini nilipotafakari vizuri, nakaamini sikuibiwa kwenye basi, bila shaka itakuwa nimeidondosha kwenye teksi wakati naiweka vizuri mara baada ya kutoa zile elfu 30, ambazo nilizitoa ili nisipate shida kutoa hela ya nauli ya basi na kutatua shida ndogondogo za njiani.

Kwakweli nilichanganyikiwa, ukizingatia ndiyo pesa niliyokuwa naitegemea katika biashara yangu niliyoendea huko na sikuwa na hela nyingine. Dereva teksi simjui wala namba yake sina, lakini nikakumbuka nilimpa namba yangu ya simu tukiwa tunaelekea Ubungo ili kuipiga wakati natafuta simu yangu. (angalia mambo yanavyoenda hapa).

Nikachukua kisimu changu, nikaangalia missed call za mwisho na kwa kuwa sikuwa nimepigiwa simu na watu wengi, niliiona namba yake mara moja, nikampigia. Huku roho ikinidunda, dereva akapokea simu na baada ya kujitambulisha kwake akanikumbuka na nikamuuliza kama ameokota bahasha kwenye gari yake!

Dereva teksi akasema hajaiona, ila baada ya kunishusha mimi, alipofika kituo cha daladala kilicho jirani na stendi ya Ubungo kuelekea Posta, alipata abiria wengine wanne (si unajua ule mtindo wa abiria wanne kuchanga buku buku) ambao aliwapakia hadi posta.

Wakati wanaelekea posta, abiria mmoja alimuuliza: “dereva, kuna abiria yoyote alipanda huma kabla yetu,?” dereva akamjibu ndiyo. “Basi naomba nikupe namba yangu, akikupigia, mpe namba yangu anaipigie,” alisema yule abiria ambaye ni mwanume wa makamu kiasi. Hata dereva teksi alipotaka kujua kulikoni, hakuambiwa.

Basi, nikamuomba dereva teksi anitumie ile namba na baada ya kunitumia nilimpigia yule kaka. Baada kumpigia simu iliita na kupokelewa. Nikajitambulisha kwake kisha akaniuliza kiasi cha pesa kilichomo na jina langu, maana kwenye ile bahasha niliweka na kitambulisho changu cha kupigia kura.

Baada ya maelezo mafupi, yule kaka akaniambia niondoe wasiwasi hela zangu zote zipo na kunieleza kuwa mara baada ya kupanda kwenye ile teksi, aliiokota bahasha hiyo chini kwenye kiti cha nyuma na hakumwambia abiria mwingine zaidi ya kumuuliza dereva teksi.

Hivyo akaniambia kuwa yeye anafanyakazi Tanesco Ubungo, nikirudi nimtafute anipe pesa zangu. Nikamwambia nimtume ndugu yangu amtafute popote alipo ili ampe hizo pesa ili mimi jikirudi kutoka Morogoro nizikute nyumbani, kaka akakataa, akasisitiza lazima anikabidhi mimi mwenywe!

Nikakubaliana naye, lakini akili ya kwanza kunijia kichwani nikahisi huu utakuwa ndiyo mwanzo wa kutongozwa, lakini yote namwachia Mungu. Hata hamu ya kukaa Morogoro sikuwa nayo, nikalazimika kugeuza siku ya pili yake kurejea Dar.

Nilipofika Dar, nikampigia simu kumtaarifu kuwa nimesharudi, akaniambia niende Ubungo Bus Stand na nikifika pale nimpigie simu atakuja nilipo, kwani ofisi zake zipo jirani hapo Tanesco Ubungo.

Kwa kuwa sikuwa najiamini, nilifuatana na ndugu yangu mmoja hadi Ubungo, nilipofika nilimpigia simu yule kaka, kwanza simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, nikaanza kuingiwa na wasi wasi huenda nimelshaingizwa mjini. Baadae nilipiga tena na kumpata, akaniambia alikuwa msikitini nimsubiri atakuja baada ya muda. Nilikaa tena kwa muda mrefu na kuendelea kuingiwa na wasiwasi zaidi, kwani alikuwa hatokei.

Wakati naanza kukata tama, mara nakaona simu inaita, kuangalia nakaona ni yule kaka, akaniambia ameshafika na ananitafuta. Nilianza kumuona mimi, nikamuelekeza nilipo akaja.

Wakati anakuja, roho ilikuwa ikinienda mbio, sikuwa na uhakika kama kweli ananiletea pesa zangu au kuna dili anataka kunichezea. Maana kwa mji wa Dar, lolote linaweza kukukuta bila kutarajia.

Alipofika, kwanza alituomba samahani kwa kuchelewa na baada ya kutambulishana pale, akanyoosha mkono wake akaniambia: HESABU PESA ZAKO DADA! Huku moyo ukinienda mbio, nikapokea na kuhesabu pesa zangu huku natetemeka. Nikakuta ZOTE ZIKO SAWA, haikupungua senti tano!!!

Na mimi kuonesha uungwana, nikahesabu shilingi 50,000 nikampa. YULE KAKA AKAZIKATAA KABISA, akasema nimpe hela ya teksi tu shilingi 4,000 aliyokuja nayo pale. Sikuamini masikio yangu. Kweli nikampa kisha tukaaga na akaondoka zake. YULE KAKA SIMJUI, HANIJUI!

Kwa dunia tuliyonayo sasa, nashindwa kuamini kama bado tuna watu waamminifu kama huyu kaka. Hakika mtu kama huyu malipo yake ni makubwa hapa duniani na kesho mbele ya Mungu. Sina cha kukupa wewe kaka, nakuombea kwa Mungu ufanikiwe katika kila jambo unalolifanya!

Hiki ni kisa cha kweli kabisa kama nilivyohadithiwa na yaliyomkuta. Je wewe, mwenzangu, unao uaminifu wa kiasi hicho?

shukurani kwa kaka mrisho abdallah.

SABA SABA JANA

Jamani sabasaba kwenye kile kitengo cha wanyama poli kusema kweli siwezi kusema chochote kwa kile nilichokiona hakika mnaweza ndugu zangu kwasababu nimeona kuna nyuki sas nyuki wale hawawezi kuleta madhara? ndio ninachojiuliza mpaka sasa jamani kama kuna mdau yeyote ambaye anaweza kuniambia chochote kuhusu hawa wadudu nawa

DUH!

Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha daladala wakafanya mazungumzo.

Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake na mwenzie akimsikiliza kwa makini,hatimaye mwenzake (jamaa wa pili) naye akasema '

Unadhani familia yako ina matatizo? ...Hayo yote ni cha mtoto mbele ya haya ya kwangu'



Basi hebu nisikilize mimi:

'Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo , hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.



Baadaye binti ya mke wangu, yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume alikuw ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja, lakini kwa vile alikua ni mtoto wa binti wa mke wangu, papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake mdogo wangu.

..Upo hapo!!.





Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe'.



SWALI.

'Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika kwa vijisenti vya matatizo wenzio wana mabilioni ya matatizo!!!!!

SHAIRI

Fataki ninaondoka , wakati umeshafikia
Nilipotoka kumbuka , wengi walinisifia
Upuuzi nilisifika , starehe kutumia
Uu ndi mwisho wangu , sasa nangoja kufa


Uzito unapungua , nahara na kutapika
Vidonda vimenijaa , salamu dada na kaka
Mwenzenu nilitanua , ushauri sikuutaka
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangoja kifo


Kwa hatayenisikia , naomba kuzingatia
Punguza kunizomea , abdallah ninaumia
Sindano kuchangia , ukimwi unapitia
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangoja kifo


Maandiko yanasema , tuachane na zinaa
Hivi sasa tunasema , kondomu ni kinga sana
Sio mimi nimesema , wenyewe mtanambia
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangja kifo


Beti tano namaliza , wahenga nawauliza
Zinaa zimekatazwa , ni sawa zimeniponza
Kondomu kuzikataza , au tuache uzwa
Kipi bora kwa sasa , kondomu au tuache fanya.

SHEIKH SULEIMANI GOROGOSI AFARIKI AJARINI LINDI


KWA HABARI ZILIZOINGIA MUDA SI MREFU KUWA KAIMU MUFTI WA TANZANIA SHEIKH SULEIMANI GOROGOSI ATUNAYE TENA DUNIANI KWA HABARI ZILIZOINGIA NI KWAMBA SHEIKH GOROGOSI AMEPATA AJALI BAADA Y GARI ALILOKUWA AMEPANDA KUPASUKA TAIRI NA KUPINDUKA .

HABARI NYINGINE NILIZOPATA NI KWAMBA MAZISHI YATAFANYIKA KWAO LINDI SAA KUMI ALAASIRI BAADA YA SWALA. MUNGU AILAZE ROHO YA SHEIKH WETU MAHALA PEMA PEPONI.

JINSI YA KUISHI NA MKE BILA MIGOGORO

Leo nitawaeleza jinsi ya kuishi na mkeo au mumeo bila kokoro cha kwanza unachopaswa kueshimu na kuelewa mwenzi wako anataka nini au anapendelea nini au kitu gani ukimfanyia analizika sana,cha pili anapendelea kula chakula cha aina gani sanasana ili umlizishe zaidi,cha tatu muwapo chumbani jaribu kumsoma muwapo kitandani sehemu gani ukimshika analidhika sana au analegea kama kapigwa shoti,kuna watu uwa awajui kuwa hata nyimbo hizi uwa zinamlidhisha mtu,jaribu kuangalia nyimbo gani ukimuwekea anaridhika zaidi ya maelezo.

NIPO KWA AJILI YA MALAVIDAVI

WADAU WANGU WA MAMBO YA MALAVIDAVI YEYOTE KWENYE MAMBO YEYOTEYANAHUSIANA NA MALAVIDAVI NAOMBA ANITUMIE EMAIL KWENYE MAIL YANGU CHINI HAPO NA NITAIPOST KAMA ILIVYO ILA ISIWE YA KUCHAFUA MAZINGIRA .85ngatunga@gmail.com.
TAARIFA YA MKUTANO WA HADHARA

Tafadhali husika na somo hilo hapo juu,
Chama cha Wananchi – CUF kinapenda kuwajulisha kuwa kitafanya mkutano wa Hadhara siku ya Jumamosi ya tarehe 27/6/2009 kuanzia saa 8:00 Mchana katika Viwanja vya Kibanda maiti. Mgeni rasmi katika Mkutano huo atakuwa ni Katibu Mkuu wa CUf Maalim Seif Shariff Hamad.
Kwa Taarifa hii wote mnaalikwa.
HAKI SAWA KWA WOTE
Salim Bimani
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma
BREEK NEWSSSSSSSSSSSSSSSS MICHAEL JACKSON AMETUTOKA
kwa habari ambazo nimezipata kutoka kwenye mitandao mbalimbali leo hii hasubuhi kwamba michael jackson atunaye,naomba jamani nanukuu sina ukweli halisi.