DUH!

Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha daladala wakafanya mazungumzo.

Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake na mwenzie akimsikiliza kwa makini,hatimaye mwenzake (jamaa wa pili) naye akasema '

Unadhani familia yako ina matatizo? ...Hayo yote ni cha mtoto mbele ya haya ya kwangu'



Basi hebu nisikilize mimi:

'Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo , hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.



Baadaye binti ya mke wangu, yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume alikuw ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja, lakini kwa vile alikua ni mtoto wa binti wa mke wangu, papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake mdogo wangu.

..Upo hapo!!.





Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe'.



SWALI.

'Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika kwa vijisenti vya matatizo wenzio wana mabilioni ya matatizo!!!!!