Fataki ninaondoka , wakati umeshafikia
Nilipotoka kumbuka , wengi walinisifia
Upuuzi nilisifika , starehe kutumia
Uu ndi mwisho wangu , sasa nangoja kufa
Uzito unapungua , nahara na kutapika
Vidonda vimenijaa , salamu dada na kaka
Mwenzenu nilitanua , ushauri sikuutaka
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangoja kifo
Kwa hatayenisikia , naomba kuzingatia
Punguza kunizomea , abdallah ninaumia
Sindano kuchangia , ukimwi unapitia
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangoja kifo
Maandiko yanasema , tuachane na zinaa
Hivi sasa tunasema , kondomu ni kinga sana
Sio mimi nimesema , wenyewe mtanambia
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangja kifo
Beti tano namaliza , wahenga nawauliza
Zinaa zimekatazwa , ni sawa zimeniponza
Kondomu kuzikataza , au tuache uzwa
Kipi bora kwa sasa , kondomu au tuache fanya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment