MSICHANA AJIFUNGUA BILA MTU YEYOTE KUFAHAMU

MSICHANA MMOJA ANAYEKADIRIWA KUWA NA MIAKA KATI YA 24 MPAKA 28 AMEJIFUNGUA SALAMA HAPO NYUMBANI KWAO TANDIKA MTAA WA MUWALE NYUMBA NO 44 TUKIO HILO LILITOKEA MAJIRA YA SAA TATU USIKU TAREHE 22/07/2009 BAADA YA MSICHANA HUYO KUJIFUNGIA NDANI BILA MTU YEYOTE YULE KUJUA CHOCHOTE KILE NA KUJIFUNGUA MSICHANA HUYO INASEMEKANA KUWA ALIKUWA AKIFANYA KAZI KWA MAMA MMOJA AITWAYE MAMA KURWA NA MASHUUDA WA TUKIO HILI WANASEMA HAKUNA HATA MTU MMOJA ALIYEKUWA AKIFAHAMUM KWAMBA HUYU MSICHANA ANGEKUWA NA MIMBA.

DAH HUYU DADA ETU NAYE KAZIDI KHA! SASA HII STYLE GANI?

OMSyvpD7AFs/Sl7w-VK7vQI/AAAAAAAAACg/R_MnCEi_-Bo/s1600-h/untitled.bmp">alt=""id="BLOGGER_PHOTO_ID_5358985560243027202" />

DAH HII NI NOMA.

MANCHESTER UNITED



kwa asiyejuwa jamani ni mpenzi wa MAN U FC mpaka naudhi yani dah!

TUNDA MAN SPACK WAJIUNGA TMK WANAUME FAMILY


JUU PICHA NI TUNDA MAN NA SPACK

KWA HABARI NILIZOZIPATA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KUWA WASANII HAO WALIOANZIA LAFAMILIA MPAKA KUJA TIPTOP CONECTION AMBAO SASA KIUJUMLA WOTE WAMEAMUA KUUNGANISHA JESHI LA TMK.WASANII WENGINE WALIOUNGA MKONO MUUNGANYIKO HUO NI CHEGE,STICKO,MADEE,NA WENGINEO WENGI.

JAMANI MAFUA YA KITI MOTO YAPO BONGO





Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, leo imetoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa hatari wa mafua makali ya nguruwe (Swine Influenza/ FLU) hapa nchini.
Wizara hiyo pia imewataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa juu ya maambukizi ya ugonjwa huo.
Tamko hilo limekuja kufuatia kubainika kuwepo kwa mgonjwa mmoja ambaye amelazwa katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili akiugua ugonjwa huo.
Akitoa tamko hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika wizarani hapo leo , Naibu Waziri katika wizara hiyo Aisha Kigoda, alisema kuwa mgonjwa aliyelazwa Muhimbili ni mwanafunzi , raia wa Uingereza aliyewasili hapa nchini kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK.Nyerere Dar es Salaam, Julai 4, mwaka huu, akitokea London, Uingereza, na ndege ya shirika la Kenya Airways, ambayo ilipitia Nairobi kabla ya kutua Tanzania.
Waziri Kigoda alisema kuwa, mgonjwa huyo ni pamoja na kundi la kwanza la wanafunzi wenzake 15 na walimu wanne. Jumla ya wanafunzi wanaotarajiwa kuja nchini ni 350, kwa ajili ya safari yao ya mafunzo na kupanda mlima Kilimanjaro wakati wa kipindi cha majira ya joto.
Alisema, mgonjwa huyo aligundulika mara moja alipowasili uwanja wa ndege Dar, na kujaza fomu zinazomtambulisha abiria yoyote mwenye dalili za ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa mgonjwa huyo baada ya kutua Dar alionekana kuwa na dalili za homa kali, mafua, kuumwa koo, kupiga chafya pamoja na mwili kuwa dhaifu.
Alisema wataalamu wa afya wa uwanja wa ndege, wakishirikiana na wataalamu wa wizara yake makao makuu, walimchukua mgonjwa huyo na kumweka katika chumba maalum na kuchukua sampuli ambazo zilipelekwa maabara iliyopo kwenye Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa na Binadamu (NIMR) ambapo vipimo vilionesha dhahiri kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na vimelea vya mafua makali ya nguruwe.
Waziri Kigoda alisema sampuli zingine zilipelekwa katika maabara inayotambuliwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) iliyopo Nairobi, Kenya, ambapo pia ilithibitika kuwa mwanafunzi huyo ana virusi vya ugonjwa huo.
Alisema mgonjwa huyo alipatiwa matibabu mara moja na kwa sasa amelazwa katika wodi maalum ya magonjwa ya kuambukiza , Muhimbili, ingawa alisema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri.
Waziri huyo alidai kuwa uchunguzi pia ulifanywa kwa wanafunzi wenzake na walimu wao na hakuna aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Taarifa za kupiga hodi kwa ugonjwa huo hapa nchini zimeonekana kuwatia hofu wananchi wengi, baada ya vyombo vya habari kuripoti juu ya kuwepo kwa mgonjwa mmoja anayeugua ugonjwa huo.

JAMANI TUJIHADHARI NA HIZI

NIMEKUTANA NA HII KWENYE MAIL YANGU JAMANI JIHADHARINI KWA WALE WENYE MAIL MSITOE AKAUNTI NAMBA ZENU KWA WATU KAMA HAWA WASANII TU HAWA WA MJINI.


VERY URGENT
FROM MR. HASSAN BILLY,
GREETINGS.

PLEASE, I WILL LIKE YOU TO CONTACT ME THROUGH MY PRIVATE EMAIL ADDRESS: (mr_hbillya2@voila.fr )

Complement of the day to you and your beloved FAmily, I apologize for this intrusion, I decided to contact you through email due to the urgency involved in this matter. Do not be astonished for receiving this mail. Please, I seek your permission and would want to get myself introduce to you. I am Mr.Hassan Billy. I work with BANK INTERNATIONAL OF BURKINA (BIB).

I need your co-operation in receiving USD9.5M that has been in a dormant account with my bank for over 6years which belongs to one of our foreign customer who died along with his entire family in a plane crash that happened in Kenya, East Africa. I will provide you with detailed informations on the modalities of this operation once I have your interest but I must say that trust flourishes business. Therefore let your conscience towards this proposal be nurtured with sincerity and I will not fail to bring to your notice that, this transaction is hitch-free risk and you should keep this transaction (TOP SECRET).

I agree that 35% of this money will be for you as a foreign partner, in respect to the provision of a foreign account, and 65% would be for me, thereafter I will visit your country for disbursement according to the percentage indicated. Remember, you must apply first to the bank as relation or next of kin of the deceased, indicating your 1) Bank name, 2) Your bank account number, 3) Your private telephone and fax number for easy and effective communication and my career as a banker, I will bring you up to date with all the informations as soon as I hear from you but If I don 't hear from you within a certain period, I will assume you are not interested.

Please, I want you to visit the website below for more informations about the plane crash and the Deceased DR.GEORGE BRUMLEY AND HIS FAMILY.

www.cnn.com/2003/WORLD/africa/07/20/kenya.crash/index.html
www.news24.com/News24/Africa/News/0,,2-11-1447_1390626,00.html

Meanwhile, If you are willing, capable and honest for this transaction, Kindly indicate your interest by sending a response to my e-mail address at: (mr_hbillya2@voila.fr )

Yours Truely,
Mr. Hassan Billy

kisa cha kweli kabisa

Nimehadithiwa kisa kimoja cha kweli na cha kustaajabisha ambacho kimeniacha na maswali mengi na mwisho nikamuuliza aliyenihadithia; “huyo jamaa hakuwa jini kweli? kisa chenyewe nimehadithiwa na dada mmoja aged between 35 – 40 ambaye hapendi nimtaje jina. Alinihadithia kama ifuatavyo:

Mambo? (naishi nae jirani), nina stori nataka nikupe, maana mimi mwenyewe nimeshangaa na mpaka sasa hivi siamini kilichotokea. Wiki iliyopita nilikwenda Morogoro, wakati naondoka hapa nyumbani (anakaa Ilala) kwenda Ubungo nilichukua teksi. Wakati naondoka nilikuwa na jumla ya shilingi 280,0000.

Nilichukua shilingi 30,000 nikaweka kwenye pochi ndogo kisha nikaweka kwenye sidiria, iliyobaki 250,000 nikaweka kwenye bahasha halafu nikaiweka kwenye mkoba wangu ambao nilipokuwa kwenye teksi, niliuweka kwenye kiti cha abiria cha nyuma.

Huyo dereva huwa namuona tu, kwani gari lake huwa analaza jirani yetu, lakini simjui vizuri. Tukiwa tunaelekea ubungo stendi, nilikumbuka simu yangu, nilipojisachi nikaona sina, lakini nilikuwa na uhakika nilipanda nayo, nikamuomba dereva aipige simu yangu ili kama imeangukia ndani ya gari niione.

Nikampa namba yangu akaipiga, kweli ikaita kutoka chini ya kiti nilichokuwa nimekaa. Nikaiokota kisha nikaiweka vizuri tukaendelea na safari yetu hadi Ubungo, tulipofika nikamlipa dereva nauli yake tukaagana. Mimi moja kwa moja kwenye basi hadi Morogoro.

Nilipofika nyumbani Morogoro, nikafungua mkoba wangu ili nitoe ile bahasha yenye 250,000, lakini sikuiona, nikajaribu kupekua vizuri kila mahali lakini wapi, moja kwa moja nikajua ile bahasha yenye pesa nimeibiwa.

Lakini nilipotafakari vizuri, nakaamini sikuibiwa kwenye basi, bila shaka itakuwa nimeidondosha kwenye teksi wakati naiweka vizuri mara baada ya kutoa zile elfu 30, ambazo nilizitoa ili nisipate shida kutoa hela ya nauli ya basi na kutatua shida ndogondogo za njiani.

Kwakweli nilichanganyikiwa, ukizingatia ndiyo pesa niliyokuwa naitegemea katika biashara yangu niliyoendea huko na sikuwa na hela nyingine. Dereva teksi simjui wala namba yake sina, lakini nikakumbuka nilimpa namba yangu ya simu tukiwa tunaelekea Ubungo ili kuipiga wakati natafuta simu yangu. (angalia mambo yanavyoenda hapa).

Nikachukua kisimu changu, nikaangalia missed call za mwisho na kwa kuwa sikuwa nimepigiwa simu na watu wengi, niliiona namba yake mara moja, nikampigia. Huku roho ikinidunda, dereva akapokea simu na baada ya kujitambulisha kwake akanikumbuka na nikamuuliza kama ameokota bahasha kwenye gari yake!

Dereva teksi akasema hajaiona, ila baada ya kunishusha mimi, alipofika kituo cha daladala kilicho jirani na stendi ya Ubungo kuelekea Posta, alipata abiria wengine wanne (si unajua ule mtindo wa abiria wanne kuchanga buku buku) ambao aliwapakia hadi posta.

Wakati wanaelekea posta, abiria mmoja alimuuliza: “dereva, kuna abiria yoyote alipanda huma kabla yetu,?” dereva akamjibu ndiyo. “Basi naomba nikupe namba yangu, akikupigia, mpe namba yangu anaipigie,” alisema yule abiria ambaye ni mwanume wa makamu kiasi. Hata dereva teksi alipotaka kujua kulikoni, hakuambiwa.

Basi, nikamuomba dereva teksi anitumie ile namba na baada ya kunitumia nilimpigia yule kaka. Baada kumpigia simu iliita na kupokelewa. Nikajitambulisha kwake kisha akaniuliza kiasi cha pesa kilichomo na jina langu, maana kwenye ile bahasha niliweka na kitambulisho changu cha kupigia kura.

Baada ya maelezo mafupi, yule kaka akaniambia niondoe wasiwasi hela zangu zote zipo na kunieleza kuwa mara baada ya kupanda kwenye ile teksi, aliiokota bahasha hiyo chini kwenye kiti cha nyuma na hakumwambia abiria mwingine zaidi ya kumuuliza dereva teksi.

Hivyo akaniambia kuwa yeye anafanyakazi Tanesco Ubungo, nikirudi nimtafute anipe pesa zangu. Nikamwambia nimtume ndugu yangu amtafute popote alipo ili ampe hizo pesa ili mimi jikirudi kutoka Morogoro nizikute nyumbani, kaka akakataa, akasisitiza lazima anikabidhi mimi mwenywe!

Nikakubaliana naye, lakini akili ya kwanza kunijia kichwani nikahisi huu utakuwa ndiyo mwanzo wa kutongozwa, lakini yote namwachia Mungu. Hata hamu ya kukaa Morogoro sikuwa nayo, nikalazimika kugeuza siku ya pili yake kurejea Dar.

Nilipofika Dar, nikampigia simu kumtaarifu kuwa nimesharudi, akaniambia niende Ubungo Bus Stand na nikifika pale nimpigie simu atakuja nilipo, kwani ofisi zake zipo jirani hapo Tanesco Ubungo.

Kwa kuwa sikuwa najiamini, nilifuatana na ndugu yangu mmoja hadi Ubungo, nilipofika nilimpigia simu yule kaka, kwanza simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, nikaanza kuingiwa na wasi wasi huenda nimelshaingizwa mjini. Baadae nilipiga tena na kumpata, akaniambia alikuwa msikitini nimsubiri atakuja baada ya muda. Nilikaa tena kwa muda mrefu na kuendelea kuingiwa na wasiwasi zaidi, kwani alikuwa hatokei.

Wakati naanza kukata tama, mara nakaona simu inaita, kuangalia nakaona ni yule kaka, akaniambia ameshafika na ananitafuta. Nilianza kumuona mimi, nikamuelekeza nilipo akaja.

Wakati anakuja, roho ilikuwa ikinienda mbio, sikuwa na uhakika kama kweli ananiletea pesa zangu au kuna dili anataka kunichezea. Maana kwa mji wa Dar, lolote linaweza kukukuta bila kutarajia.

Alipofika, kwanza alituomba samahani kwa kuchelewa na baada ya kutambulishana pale, akanyoosha mkono wake akaniambia: HESABU PESA ZAKO DADA! Huku moyo ukinienda mbio, nikapokea na kuhesabu pesa zangu huku natetemeka. Nikakuta ZOTE ZIKO SAWA, haikupungua senti tano!!!

Na mimi kuonesha uungwana, nikahesabu shilingi 50,000 nikampa. YULE KAKA AKAZIKATAA KABISA, akasema nimpe hela ya teksi tu shilingi 4,000 aliyokuja nayo pale. Sikuamini masikio yangu. Kweli nikampa kisha tukaaga na akaondoka zake. YULE KAKA SIMJUI, HANIJUI!

Kwa dunia tuliyonayo sasa, nashindwa kuamini kama bado tuna watu waamminifu kama huyu kaka. Hakika mtu kama huyu malipo yake ni makubwa hapa duniani na kesho mbele ya Mungu. Sina cha kukupa wewe kaka, nakuombea kwa Mungu ufanikiwe katika kila jambo unalolifanya!

Hiki ni kisa cha kweli kabisa kama nilivyohadithiwa na yaliyomkuta. Je wewe, mwenzangu, unao uaminifu wa kiasi hicho?

shukurani kwa kaka mrisho abdallah.

SABA SABA JANA

Jamani sabasaba kwenye kile kitengo cha wanyama poli kusema kweli siwezi kusema chochote kwa kile nilichokiona hakika mnaweza ndugu zangu kwasababu nimeona kuna nyuki sas nyuki wale hawawezi kuleta madhara? ndio ninachojiuliza mpaka sasa jamani kama kuna mdau yeyote ambaye anaweza kuniambia chochote kuhusu hawa wadudu nawa