DUH!

Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha daladala wakafanya mazungumzo.

Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake na mwenzie akimsikiliza kwa makini,hatimaye mwenzake (jamaa wa pili) naye akasema '

Unadhani familia yako ina matatizo? ...Hayo yote ni cha mtoto mbele ya haya ya kwangu'



Basi hebu nisikilize mimi:

'Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo , hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.



Baadaye binti ya mke wangu, yaani binti yangu wa kambo alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume alikuw ndugu yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja, lakini kwa vile alikua ni mtoto wa binti wa mke wangu, papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake mdogo wangu.

..Upo hapo!!.





Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kua shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe'.



SWALI.

'Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia? Acha kulalamika kwa vijisenti vya matatizo wenzio wana mabilioni ya matatizo!!!!!

SHAIRI

Fataki ninaondoka , wakati umeshafikia
Nilipotoka kumbuka , wengi walinisifia
Upuuzi nilisifika , starehe kutumia
Uu ndi mwisho wangu , sasa nangoja kufa


Uzito unapungua , nahara na kutapika
Vidonda vimenijaa , salamu dada na kaka
Mwenzenu nilitanua , ushauri sikuutaka
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangoja kifo


Kwa hatayenisikia , naomba kuzingatia
Punguza kunizomea , abdallah ninaumia
Sindano kuchangia , ukimwi unapitia
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangoja kifo


Maandiko yanasema , tuachane na zinaa
Hivi sasa tunasema , kondomu ni kinga sana
Sio mimi nimesema , wenyewe mtanambia
Uu ndio mwisho wangu , sasa nangja kifo


Beti tano namaliza , wahenga nawauliza
Zinaa zimekatazwa , ni sawa zimeniponza
Kondomu kuzikataza , au tuache uzwa
Kipi bora kwa sasa , kondomu au tuache fanya.

SHEIKH SULEIMANI GOROGOSI AFARIKI AJARINI LINDI


KWA HABARI ZILIZOINGIA MUDA SI MREFU KUWA KAIMU MUFTI WA TANZANIA SHEIKH SULEIMANI GOROGOSI ATUNAYE TENA DUNIANI KWA HABARI ZILIZOINGIA NI KWAMBA SHEIKH GOROGOSI AMEPATA AJALI BAADA Y GARI ALILOKUWA AMEPANDA KUPASUKA TAIRI NA KUPINDUKA .

HABARI NYINGINE NILIZOPATA NI KWAMBA MAZISHI YATAFANYIKA KWAO LINDI SAA KUMI ALAASIRI BAADA YA SWALA. MUNGU AILAZE ROHO YA SHEIKH WETU MAHALA PEMA PEPONI.

JINSI YA KUISHI NA MKE BILA MIGOGORO

Leo nitawaeleza jinsi ya kuishi na mkeo au mumeo bila kokoro cha kwanza unachopaswa kueshimu na kuelewa mwenzi wako anataka nini au anapendelea nini au kitu gani ukimfanyia analizika sana,cha pili anapendelea kula chakula cha aina gani sanasana ili umlizishe zaidi,cha tatu muwapo chumbani jaribu kumsoma muwapo kitandani sehemu gani ukimshika analidhika sana au analegea kama kapigwa shoti,kuna watu uwa awajui kuwa hata nyimbo hizi uwa zinamlidhisha mtu,jaribu kuangalia nyimbo gani ukimuwekea anaridhika zaidi ya maelezo.

NIPO KWA AJILI YA MALAVIDAVI

WADAU WANGU WA MAMBO YA MALAVIDAVI YEYOTE KWENYE MAMBO YEYOTEYANAHUSIANA NA MALAVIDAVI NAOMBA ANITUMIE EMAIL KWENYE MAIL YANGU CHINI HAPO NA NITAIPOST KAMA ILIVYO ILA ISIWE YA KUCHAFUA MAZINGIRA .85ngatunga@gmail.com.
TAARIFA YA MKUTANO WA HADHARA

Tafadhali husika na somo hilo hapo juu,
Chama cha Wananchi – CUF kinapenda kuwajulisha kuwa kitafanya mkutano wa Hadhara siku ya Jumamosi ya tarehe 27/6/2009 kuanzia saa 8:00 Mchana katika Viwanja vya Kibanda maiti. Mgeni rasmi katika Mkutano huo atakuwa ni Katibu Mkuu wa CUf Maalim Seif Shariff Hamad.
Kwa Taarifa hii wote mnaalikwa.
HAKI SAWA KWA WOTE
Salim Bimani
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma
BREEK NEWSSSSSSSSSSSSSSSS MICHAEL JACKSON AMETUTOKA
kwa habari ambazo nimezipata kutoka kwenye mitandao mbalimbali leo hii hasubuhi kwamba michael jackson atunaye,naomba jamani nanukuu sina ukweli halisi.